<link rel="stylesheet" href="styles.f3b1fba60ec7970c.css">
The Catholic University of Eastern Africa crestCUEA Digital RepositoryOpen access research, theses & scholarly works

UCHANGANUZI WA TASWIRA YA VIJANA WA KIUME KATIKA RIWAYA ZA NJOZI YAPATA MTENZI NA UTELEZI

dc.contributor.authorOPICHO N PERPETUA
dc.date.accessioned2026-11-17T18:36:33Z
dc.date.issued2026-11-17
dc.descriptionTHESIS
dc.description.abstractVijana wa kiume ni kundi muhimu katika jamii linalopitia kipindi cha kujenga utambulisho na kujiandaa kwa majukumu ya utu uzima huku likikabiliwa na matarajio mbalimbali ya kijamii kuhusu uanaume. Hata hivyo, matarajio haya hayatoshelezwi kila mara kutokana na changamoto za kifamilia, kijamii, kiuchumi na kielimu zinazowakabili vijana wa kiume. Aidha, tafiti zilizopo hazijachanganua kwa pamoja namna vijana wa kiume wanavyosawiriwa, changamoto zinazowakumba na nafasi ya jamii katika kuwakuza katika Njozi Yapata Mtenzi (2018) na Utelezi (2023). Utafiti huu ulilenga kuchanganua taswira ya vijana wa kiume katika riwaya hizo teule. Madhumuni mahususi yalikuwa: kubainisha jinsi vijana wa kiume walivyosawiriwa; kujadili changamoto zinazowakumba; na kuchanganua mchango wa jamii katika kuwakuza vijana wa kiume katika riwaya hizo. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uwezo-Mkuu wa Kiume iliyoasisiwa na R. W. Connell katika miaka ya 1980 na kufafanuliwa zaidi katika Gender and Power (1987). Mihimili ya nadharia hii ilizingatia mchango wa matarajio ya kijamii, mazingira, mahusiano na majukumu ya kijinsia katika ujenzi wa uanaume. Utafiti ulitumia muundo wa kimaelezo. Kundi lengwa lilikuwa riwaya kumi za Kiswahili zilizoandikwa na Mwenda Mbatia, ambapo Njozi Yapata Mtenzi (2018) na Utelezi (2023) ziliteuliwa kimakusudi kama sampuli. Data zilikusanywa kwa kusoma riwaya hizo kwa makini, kunukuu vifungu vinavyohusiana na malengo ya utafiti na kuvipanga kwa kutumia orodha ya uthibitishaji (checklist). Uchanganuzi wa data ulikuwa wa kimaelezo na kimaudhui kwa kuongozwa na malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia. Utafiti uligundua kuwa vijana wa kiume wamesawiriwa kama wasomi, wenye bidii, ujasiri, utu, ndoto na matarajio makubwa, vipawa vya michezo, ustahimilivu pamoja na ufahamu wa kisiasa na kijamii, huku baadhi yao wakisawiriwa kupitia matumizi ya mihadarati, wizi, ukatili na kupenda raha. Utafiti pia ulibaini changamoto mbalimbali zikiwemo vifo, ukosefu wa ajira, ufisadi, unyanyasaji, mihadarati, uongozi mbaya, ubaguzi, usaliti, utelekezwaji, shinikizo la marika, umaskini na changamoto za elimu. Aidha, jamii imebainika kuwa na mchango chanya kupitia malezi, elimu, ushauri, fursa na mifano ya kuigwa, na mchango hasi kupitia uzembe, ufisadi, utelekezwaji na mienendo inayowapotosha vijana. Hitimisho la utafiti ni kuwa taswira ya vijana wa kiume hujengwa na mwingiliano wa sifa binafsi, matarajio ya kijamii, mazingira na mahusiano ya kijamii. Mihimili ya Nadharia ya Uwezo-Mkuu wa Kiume imefaa katika kueleza ujenzi wa uanaume, changamoto za vijana wa kiume na nafasi ya jamii katika kuwakuza. Utafiti umejibu maswali yote matatu na una umuhimu katika Fasihi ya Kiswahili kwa kupanua mjadala kuhusu vijana wa kiume, uanaume na ujenzi wa wahusika katika riwaya. Kufuatia matokeo hayo, inapendekezwa kuwa tafiti zaidi zichunguze taswira ya vijana wa kiume na ujenzi wa uanaume katika riwaya nyingine za Kiswahili na tanzu nyingine za fasihi, pamoja na tafiti linganishi kuhusu namna waandishi wa kike na wa kiume wanavyowasawiri vijana wa kiume.
dc.identifier.urihttps://repository.cuea.edu/handle/123456789/779
dc.language.isoother
dc.publisherTHE CATHOLIC UNIVERSITY OF EASTERN AFRICA
dc.subjectUchanganuzi wa Taswira
dc.subjectVijana wa Kiume
dc.subjectRiwaya za Kiswahili
dc.subjectUwakilishaji wa Kijinsia
dc.subjectUanaume
dc.subjectUtambulisho wa Kiume
dc.subjectVijana katika Fasihi
dc.subjectUchanganuzi wa Kifasihi
dc.subjectUhakiki wa Riwaya
dc.subjectMaudhui ya Riwaya
dc.subjectWahusika wa Kiume
dc.subjectNafasi ya Vijana katika Jamii
dc.subjectMahusiano ya Kijamii
dc.subjectMabadiliko ya Kijamii
dc.subjectFasihi ya Kiswahili
dc.subjectNjoozi Yapata Mtenzi
dc.subjectUtelezi.
dc.titleUCHANGANUZI WA TASWIRA YA VIJANA WA KIUME KATIKA RIWAYA ZA NJOZI YAPATA MTENZI NA UTELEZI
dc.typeThesis

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
TASNIFU FINAL 21-09.pdf
Size:
1.09 MB
Format:
Adobe Portable Document Format