<link rel="stylesheet" href="styles.f3b1fba60ec7970c.css">
The Catholic University of Eastern Africa crestCUEA Digital RepositoryOpen access research, theses & scholarly works

UCHAMBUZI WA MAWASILIANO YA UHIFADHI WA MAZINGIRA KATIKA VIPINDI VYA SHAMBA SHAPE-UP NA CITIZEN PLANET VYA RUNINGA YA CITIZEN NCHINI KENYA

dc.contributor.authorNJAU WAMBUI JOYCE
dc.date.accessioned2026-11-19T16:56:23Z
dc.date.issued2026-11-19
dc.descriptionTHESIS
dc.description.abstractUtafiti huu ulichambua mawasiliano ya uhifadhi wa mazingira katika vipindi vya Shamba Shape-Up na Citizen Planet vya Runinga ya Citizen nchini Kenya. Utafiti ulilenga kubainisha masuala ya uhifadhi wa mazingira yanayowasilishwa, kuchanganua changamoto za kimazingira zinazoibuliwa na kuchunguza mikakati ya kimawasiliano inayotumiwa katika kuwasilisha ujumbe wa uhifadhi wa mazingira. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhakiki- Ikolojia ambayo ilianza kujengeka katika miaka ya 1970 na William Rueckert. Baadaye, nadharia hii iliendelezwa na wataalamu mbalimbali, wakiwemo Cheryll Glotfelty na Fromm (1996), inayosisitiza kuchunguza uhusiano na utegemeano kati ya binadamu na mazingira, athari za shughuli za binadamu kwa mifumo ikolojia na wajibu wa binadamu katika uhifadhi wa mazingira. Utafiti ulitumia mkabala wa kimaelezo na muundo wa uchambuzi wa nyaraka na maudhui, huku sampuli ya makusudi ikitumika kuteua vipindi vyenye maudhui ya kimazingira. Matokeo yalibainisha kuwa vipindi hivyo vinawasilisha masuala ya uhifadhi wa misitu na upandaji miti, uhifadhi wa udongo na maji, kilimo hifadhi, bioanuwai, usimamizi wa taka, nishati endelevu na mabadiliko ya tabianchi. Pia vilibainisha changamoto za ukataji miti, uchafuzi, mmomonyoko wa udongo, ukame, kupungua kwa rutuba ya udongo na upotevu wa bioanuwai. Mikakati ya mawasiliano iliyobainika ni pamoja na lugha rahisi, mahojiano ya wataalamu, maonesho ya vitendo, ushuhuda wa jamii, simulizi, picha na vielelezo. Utafiti ulihitimisha kuwa vipindi hivi ni majukwaa muhimu ya mawasiliano ya mazingira na unapendekeza kuimarishwa kwa maudhui ya mazingira, ushiriki wa jamii na ushirikiano kati ya vyombo vya habari, wataalamu na taasisi za mazingira ili kukuza uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za asili nchini Kenya.
dc.identifier.urihttps://repository.cuea.edu/handle/123456789/822
dc.language.isoother
dc.publisherTHE CATHOLIC UNIVERSITY OF EASTERN AFRICA
dc.subjectMawasiliano ya Uhifadhi wa Mazingira
dc.subjectUhifadhi wa Mazingira
dc.subjectMawasiliano ya Kimazingira
dc.subjectVipindi vya Televisheni
dc.subjectUchanganuzi wa Mawasiliano
dc.subjectUhamasishaji wa Mazingira
dc.subjectElimu ya Mazingira
dc.subjectUtangazaji wa Televisheni
dc.subjectUandishi wa Habari za Mazingira
dc.subjectMawasiliano ya Umma
dc.subjectMabadiliko ya Tabianchi
dc.subjectUendelevu wa Mazingira
dc.subjectShamba Shape-Up
dc.subjectCitizen Planet
dc.subjectCitizen TV
dc.subjectKenya.
dc.titleUCHAMBUZI WA MAWASILIANO YA UHIFADHI WA MAZINGIRA KATIKA VIPINDI VYA SHAMBA SHAPE-UP NA CITIZEN PLANET VYA RUNINGA YA CITIZEN NCHINI KENYA
dc.typeThesis

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Pendekezo la Utafiti - Joice Njau Edited (2) (Edited) (3).pdf
Size:
1.58 MB
Format:
Adobe Portable Document Format