UCHANGANUZI WA MASUALA MTAMBUKO NA LUGHA KATIKA MASHAIRI TEULE YA NUHU BAKARI KWENYE JUKWAA LA MTANDAO LA VIUSASA, KENYA.

dc.contributor.authorCATHERINE K. ABUYA
dc.date.accessioned2026-11-03T19:14:30Z
dc.date.available2026-11-03T19:14:30Z
dc.date.issued2026-11-03
dc.descriptionTHESIS
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia masuala mtambuko na lugha katika mashairi teule ya Nuhu Bakari yaliyowasilishwa kwenye jukwaa la mtandao la VIUSASA. Masuala mtambuko ni masuala yaliyovuka mipaka ya dhamira moja na kugusa nyanja nyingi za maisha kwa wakati mmoja. Mshairi Nuhu Bakari ni maarufu kwa ubunifu wake wa mashairi yenye ukwasi wa lugha. Mashairi ya Nuhu Bakari huakisi masuala mtambuko na lugha yenye uketo wa kisanaa. Husawiri kwa ukwasi wa kina lugha ya Kiswahili kwa kugusia masuala ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kujadili masuala mtambuko katika mashairi teule ya Nuhu Bakari na kuchunguza namna Nuhu Bakari alivyotumia lugha kuwasilisha masuala mtambuko katika mashairi yake. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uhalisia wa Kijamii kwa mujibu wa Lucas’z (2021) na Nadharia ya Umitindo kwa mujibu wa Leech na Short (1981). Muundo wa utafiti ni wa kimaelezo. Eneo la utafiti ni jukwaa la mtandao la VIUSASA. Kikundi lengwa cha utafiti ni mashairi simulizi ya Nuhu Bakari yaliyoghaniwa katika miezi ya Juni hadi Novemba 2024. Sampuli ya utafiti ni mashairi kumi na mawili yaliyoteuliwa kimakusudi kwa misingi ya uanuwai wa masuala mtambuko yaliyomo. Data zilikusanywa kwa kusikiliza kwa makini na kuyanakili mashairi ya Nuhu Bakari yaliyoghaniwa katika miezi ya Juni hadi Novemba 2024. Uchanganuzi wa data utafanywa kimaelezo. Data za kila lengo la utafiti ziliainishwa. Mtafiti alibuni mada ndogondogo kutokana na dhamira mbalimbali zilizojitokeza katika mashairi yaliyoteuliwa. Data za kila lengo la utafiti zilifasiriwa, mtafiti alinukuu madondoo na kuyajadili kwa kina huku akiongozwa na nadharia za utafiti. Mawazo ya wataalamu waliotangulia yalirejelewa pia ili kuimarisha mjadala. Matokeo yalibainisha kuwa mashairi ya Nuhu Bakari kwenye VIUSASA yanajadili masuala sita mtambuko. Haya ni usalama, uchumi, ulaghai, siasa, elimu na haki za vijana, jinsia, ndoa na dini. Masuala hayo yanaingiliana na kuakisi matukio halisi ya Kenya. Miongoni mwayo ni machafuko ya Baringo, Mswada wa Fedha wa 2024, maandamano ya Gen-Z, kashfa ya mbolea ghushi, na tukio la Butere. Mbinu ya ithibati tatu imethibitisha uhusiano huu, ikiimarisha Nadharia ya Uhalisia wa Kijamii. Kimtindo, mashairi haya yalitumia mbinu kumi na nne za kisanaa. Mbinu hizo ni pamoja na; sitiari, majazi na lakabu, takriri, nidaa, maswali ya balagha, misemo na nahau, tamathali za kidini, kuchanganya ndimi na kuhamisha msimbo, tashbiha, tashihisi, chuku, ritifaa, kinaya na tasfida. Mbinu hizi zinaongozwa na Umitindo. Zinaunganika kuimarisha uzito wa kihisia na kijamii wa ujumbe. Utafiti huu unatarajiwa kuwanufaisha wasomi, waandishi wa mashairi, wanaoghani mashairi katika vyombo vya habari, na waunda mitaala ya elimu nchini Kenya.
dc.identifier.urihttps://repository.cuea.edu/handle/123456789/721
dc.language.isoother
dc.publisherTHE CATHOLIC UNIVERSITY OF EASTERN AFRICA
dc.subjectUchanganuzi wa lugha
dc.subjectmasuala mtambuko
dc.subjectushairi wa Kiswahili
dc.subjectmashairi teule
dc.subjectNuhu Bakari
dc.subjectlugha ya kishairi
dc.subjecttamathali za usemi
dc.subjectdhamira za ushairi
dc.subjectfasihi simulizi
dc.subjectfasihi andishi
dc.subjectmitandao ya kijamii
dc.subjectViusasa
dc.subjectKenya
dc.titleUCHANGANUZI WA MASUALA MTAMBUKO NA LUGHA KATIKA MASHAIRI TEULE YA NUHU BAKARI KWENYE JUKWAA LA MTANDAO LA VIUSASA, KENYA.
dc.typeThesis

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
CATHERINES_THESIS_ (1_October_2026).pdf
Size:
1.6 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description: