UCHAMBUZI WA MAWASILIANO YA UHIFADHI WA MAZINGIRA KATIKA VIPINDI VYA SHAMBA SHAPE-UP NA CITIZEN PLANET VYA RUNINGA YA CITIZEN NCHINI KENYA
Loading...
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
THE CATHOLIC UNIVERSITY OF EASTERN AFRICA
DOI
Abstract
Utafiti huu ulichambua mawasiliano ya uhifadhi wa mazingira katika vipindi vya Shamba Shape-Up na Citizen Planet vya Runinga ya Citizen nchini Kenya. Utafiti ulilenga kubainisha masuala ya uhifadhi wa mazingira yanayowasilishwa, kuchanganua changamoto za kimazingira zinazoibuliwa na kuchunguza mikakati ya kimawasiliano inayotumiwa katika kuwasilisha ujumbe wa uhifadhi wa mazingira. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhakiki- Ikolojia ambayo ilianza kujengeka katika miaka ya 1970 na William Rueckert. Baadaye, nadharia hii iliendelezwa na wataalamu mbalimbali, wakiwemo Cheryll Glotfelty na Fromm (1996), inayosisitiza kuchunguza uhusiano na utegemeano kati ya binadamu na mazingira, athari za shughuli za binadamu kwa mifumo ikolojia na wajibu wa binadamu katika uhifadhi wa mazingira. Utafiti ulitumia mkabala wa kimaelezo na muundo wa uchambuzi wa nyaraka na maudhui, huku sampuli ya makusudi ikitumika kuteua vipindi vyenye maudhui ya kimazingira. Matokeo yalibainisha kuwa vipindi hivyo vinawasilisha masuala ya uhifadhi wa misitu na upandaji miti, uhifadhi wa udongo na maji, kilimo hifadhi, bioanuwai, usimamizi wa taka, nishati endelevu na mabadiliko ya tabianchi. Pia vilibainisha changamoto za ukataji miti, uchafuzi, mmomonyoko wa udongo, ukame, kupungua kwa rutuba ya udongo na upotevu wa bioanuwai. Mikakati ya mawasiliano iliyobainika ni pamoja na lugha rahisi, mahojiano ya wataalamu, maonesho ya vitendo, ushuhuda wa jamii, simulizi, picha na vielelezo. Utafiti ulihitimisha kuwa vipindi hivi ni majukwaa muhimu ya mawasiliano ya mazingira na unapendekeza kuimarishwa kwa maudhui ya mazingira, ushiriki wa jamii na ushirikiano kati ya vyombo vya habari, wataalamu na taasisi za mazingira ili kukuza uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za asili nchini Kenya.
Description
THESIS
Keywords
Mawasiliano ya Uhifadhi wa Mazingira , Uhifadhi wa Mazingira , Mawasiliano ya Kimazingira , Vipindi vya Televisheni , Uchanganuzi wa Mawasiliano , Uhamasishaji wa Mazingira , Elimu ya Mazingira , Utangazaji wa Televisheni , Uandishi wa Habari za Mazingira , Mawasiliano ya Umma , Mabadiliko ya Tabianchi , Uendelevu wa Mazingira , Shamba Shape-Up , Citizen Planet , Citizen TV , Kenya.
